Friday, February 20, 2009

KILA LAHERI TAIFA STARS IVORY COAST.

Taifa Stars,sisi Watanzania wote tupo pamoja nanyi katika safari yenu ya kuliwania kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani.Tunawaombea kila laheri ili muweze kuliwakilisha vema Taifa letu katika michuano hiyo mipya kabisa katika medani ya soka katika Afrika.Tulio wengi tunaamini kuwa mnaweza maana mpaka kufika hatua hiyo kwa kweli safari ilikuwa ndefu sana.
Kitu muhimu tunachowakumbusha watanzania wenzetu ni kuwa kwa kweli lazima muelewe kuwa huko mmekwenda kuwakilisha Taifa hivyo kwa njia moja au nyingine mko vitani ingawa si vita vya vifaru na mizinga bali vitavya mchezo wa soka lakini hiyo ni vita.Jitahidini kadri ya uwezo wenu mpambane kadri ya ujuzi wenu wote mliopewa na mwalimu na huku mkijua kuwa watanzania wote wapo nyuma yenu.
Kitu muhimu ni ushindi ingawa tupo tayari kuyapokea matokeo yoyote yale.
TUNA UHAKIKA KUWA MNAWEZA MAANA MPAKA KUFIKIA HAPO MLIPO KAMA NILIVYOKWISHA SEMA NI KUW MMEONYESHA KUW NINYI MU WAZURI KAMA HAO WENGINE!
Nahodha Nsajigwa hakikisha kuwa timu yako chini ya uongozi wako ndani ya kiwanja inakuwa na nidhamu wakati wote wa mchezo!Kubishana na waamuzi bila sababu ya msingi hakutaweza kutusaidia hasa ikizingatiwa kuw waamuzi wao ndiyo watoa maamuzi ya mwisho hata kama wachezaji hawakubaliani nayo.Nimekutaja nahodha kuwa unawajibika kuongoza nidhamu hasa tukumbukapo matukio ya nyuma pale tunapolalamika hata kama mwamuzi amepotoka lakini hkuna sababu ya kubishana naye sana kwani matokeo yake ni kadi na hiyo itapunguza ngu ya timu ingawaje wakayi mwingine inakuwa kichocheo cha timu kupigana kwa nguvu hadi mwisho baada ya kuijikuta kuwa tupo pungufu.Tuache hasira tuzingatie nidhamu tuwe na umoja tucheze kwa pamoja kama timu kama msemo wetu wa kiswahili usemavyo kuw umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu!
Tuna hakika kuwa viongozi wenu wamewaeleza na kuwajulisha majukumu yenu na mipaka yenu.
Hakika STARS KAMA MKIAMUA NA NINADHANI HIVYO KUWA MUMEAMUA BASI MTAWEZA NA INSHALAH KOMBE LITATUA KATIKA ARDHI HII YA BONGO!BRAVO TAIFA STARS ALUTA KONTINUA!TUPO PAMOJA NANYI.MUNGU IBARIKI TANZANIA MUNGU IBARIKI TAIFA STARS.

Monday, February 16, 2009

YANGA AFRIKA MKIAMUA MNAWEZA KULIANGUSHA KABATI!

Yanga kazi ndo kwanza imeanza.Lakini msitishike sana na hii timu pia lakini msijiamini sana eti kwa kuwa mna usajili wa bei mabaya!Usajili wenu kwa timukama ya Waarabu hawa wao pesa ya wachezaji wenu wote mlioitumia kwenye usajili wao ni ya kununulia mchezajimmoja tu Flavio wa Angola! Muhimu hapa ni kujitambua na kujielewa pia kufahamu kuwa lazima mfanye maandalizi ya maana toka sasa ili kuwezakukabiliana nao hawa jamaa.Maandalizi yawe ya maana na wala si ya zima moto.Mfanye maandalizi kwelikweli na wala si mchezo na wala si vinginevyo!.Najua ni vigumu kuyatekeleza mambo yote mawili yaani kuacha woga mbele ya hawa jamaa na pia kujiamini kupita kiasi mbele ya hawa jamaa.Lakini mkiyatafakari haya kwa kina basi mtawezakujielewa ni jinsi gani mikakati yenu mtakavyoipanga kuwezakuwakabili Waarabu hawa.Lakini suala la kufungika kwa hawa jamaa ni kitu kinachowezekena kabisa iwapo mtaamua.Lakini ninyi wachezaji mkishikamana na kocha wenu nina hakika mnaweza.Hakika mimi nina hakika mnaweza.
Ushauri wangu kwenu ni huu.Najua kuwa viongozi wenu karibu wote ni waoga na lazima watakuwa na mchecheto sana wa kupambana na Waarabu wale.Cha muhimu wala msiwasikilize,bali ninyi jinsi mnavyojiamini ni hivyo mtakavyoweza kuwafunga Waarabu wale.Kuanzia sasa jitumeni sana mafunzo na mazoezi ya mwalimu na lazima mjione kuwa mnaweza.Viongozi wenu kama nilivyosemani waoga.Watakuja na visingizio kibao ili hata mkipoteza mechi muonekane kuwa ninyi si lolote kwa waarabu wale. Kuwa mbona eti imezoeleka siku zote ninyi ni wateja kwao la hasha hilo likataeni safari hii kwa kuwaonyesha kuwamnaweza!Sasa basi lazima hapamuwaumbue viongozi ingawa najua kuwa mwisho wa siku baada ya ushindi watakuja na majigambo mengi ya kuwa ohoo hii ndo Yanga Afrika bwana tumeshikamana tumekuwa kitu kimoja tumeshinda.Nawahakikishia kuwa kama mtashinda mjue wazi kuwa ushindi huo utakuwa umetokana na juhudi zenu ninyi kama wachezaji na si vinginevyo.Hapa nasisitiza tena kuwa viongozi wenu tayari wamekwishaanza kuiogopa hiyo mechi ,lakini kwa jinsi ninavyokiona kikosi chenu hakika kama mtaamua ninyi wenyewe kweli kabisa mnaweza!Yanga wakati ndiyo huu.Waonesheni Watanzania na wapenda soka kwa ujumla kuwa mnaweza!Wakati ndiyo huu!Kila laheri DarYanga Afrika wawakilishi pekee wa Tanzania mliosalia mashindanoni.

Friday, February 06, 2009

JE TUMEMUELEWA MAMA ANNA TIBAIJUKA?

Kwa waliongalia kipindi cha TV cha Chanel Ten kinachojulikana kama "Je Tutafika kinachoendeshwa na mzee wetu Makwaia Wa Kuhenga akimhoji mama Tibaijuka kuhusu mauaji ya Maalbino nchini mwetu,sijui kama Watanzania wenzangu tulimuelewa vizuri yule mama wa Kitanzania msomi aliyebobea na mwenye kuheshimika sana Kimataifa.Napenda kumpongeza mama kwa jinsi alivyoweza kuisaidia jamii ya Watanzania kupitia kipindi kile ni kwa namna gani tutaweza kuzuia mauaji ya ndugu zetu Maalbino wasio na hatia.

Ameongea mambo ambayo hakuna hata mmoja wetu kuwa aliwahi kuwaza hata siku moja kuwa je ni njia gani tuweze kutafuta ilituweze kuzuia mauaji hayo?

Sina ya kuongea mengi lakini kama Chanel Ten wataweza kukirudia kile kipindi mara kwa mara ili Watawala wetu na Watanzania kwa ujumla tuweze kupata somo alilotoa yule mama wa Muleba ambaye anaishi na kuutumikia ulimwengu huu huko New York.

Mama Hongera sana kwa kweli umenikuna sana na nilikuelewa sana sana.Hakika tunatakiwa tuache kabisa kile ulichokiita kuwa "Stroke Brush Conclutions" kama sijakosea.Na pia kuwa kama ulivyosema kuwa lazima mtu anaposema kuwa amefanya utafiti basi uwe utafiti na si vinginevyo!

Mama somo lile ni la maana sana.Wasiwasi wangu je tumelielewa?Tujitahidi kwa bidii na maarifa tulielewe somo lile!Mzee Makwaia hongera kwa mumleta mama Anna kututatulia ili tupate ufumbuzi wa kuwakomesha hawa washenzi wasiostaraabika kwa kufikiri mawazo ya kipumbavu kuwa utajiri utatokana na viungo vya binadamu wenzetu Maalbino.Narudia tena kama tutayafuata yale aliyosema huyu mama basi tutafanikiwa kwa kiasi kikubwa kukomesha kabisa mauaji ya ndugu zetu hawa jamani.Tukumbuke kuwa thamaniya binadamu haiwezi kufananishwa na kitu chochote kile.Asante.

Friday, December 26, 2008

WATANZANIA NA HALI NGUMU YA MAISHA.

Watanzania jamani kadri miaka inavyokwenda ndiyo hali ya maisha kwa sisi tulio wengi inavyozidi kuwa mbaya,huku vikundi vya watu wachache ao wakineemeka kupitia migongo ya walala hoi ambao ndiyo wengi katika taifa letu hili linalojulikana kama changa kiuchumi lakini lenye kila raslimali za kutufanya tusiwe na maisha ya kuigiza.Nchi ina utajiri wa kutisha lakini watu wake ni masikini wa kutupwa.Je nini kifanyike ili kuondokana na hali hii jamani sisi watanzania?
Hebu angalia jinsi baadhi ya watu walivyo wabinafsi,angalia jinsi wanavyojipendelea wao wenyewe huku wakisahau mamilioni ya watanzania wenzao wanavyoteseka kwa masahibu mbalimbali yanayowakumba kila kukicha.Magonjwa,njaa,kukosa matibabu,miundo mbinu mibovu elimu duni na vitu vingi vya jinsi hiyo.Watanzania jamani bado tunaweza kuifanya nchi yetu ikawa katika hali nzuri tu kama tutakuwa wamoja na kujituma huku bila ya kusahauliana na kutengana na kubaguana.Shime tuangalie wapi tulipokosea ili tujipange upya kwa ajili ya mustakabali wa nchi yetu na wananchi wake.Karne hii ni ya kila mtu kuwa katika maisha bora mambo ya kusema kuwa eti sisi bado ni maskini kwa kweli yamepitwa na wakati hivyo inatubidi tuwe wamoja na kufanya kazi kwa kushirikiana kwa ajili ya watu wa taifa hili na nchi yote kwa ujumla.Asanteni.

Wednesday, December 24, 2008

TIMU YA TAIFA HAIWEZI KUWA BORA KAMA VILABU HAVITAKUWA BORA!

Watanzania kwa kiasi fulani tumepiga hatua katikakuelekea kwenye soka la kweli la ushindani na kutambulika kimataifa katika ulimwengu wa soka yenye akili.Tumeonyesha kuwa tunawezakutoka katika ule ujulikanao uigizwaji tu wa kikomedi katika soka na kuelekea katika hali halisi ya soka lenyewe.

Timu yetu ya Taifa kwa kiasi fulani angalau nasema kuwa angalau maana sisi ni mabingwa wa kuanzisha mikakati ya muda mrefu na mfupi lakini ambayo huwa hatuitimilizi.Kwa nini nasema hivyo ni kwa sababu ya kuja kuona kuwa kweli tumeanza na muelekeo na timu ipo vizuri kisoka lakini baadaye tena tunakuja kupote njia na kuanza kupiga hatua mia nyuma.

Mara nyingi sana tumekuwa na mipango ya maendeleo lakini inavurugika bila kutarajia.

Ninachotaka kukisema watanzania wenzangu leo ni kuwa ili timu yetu iwe nzuri basi ni vema wadau wote wa soka la Bongo wakajitolea kwa hali na mali ili kuhakikisha kuwa vilabu vinakuwa na msingi mzuri wa kisoka ili iwe chimbuko la kupata wachezaji wazuri wa timu ya taifa.Hapa lazima tuwe na mipango madhubuti ya soka katika vilabu vyetu kwa maana vilabu vyetu mpaka leo bado vinajiendesha katika enzi ya ujima kabisa kitu ambacho tunatakiwa tuondokane nacho kwa sasa.

Simba Yanga Mtibwa na vilabu vingine vyote wakati ni huu tumechelewa lakini tunaweza kufanya vizuri kama tutaamua kuwatunaanza na tunaweza.Tuanze sasa kuwa klabu na si mahala pagumzo na uswahili vilabuni huku tukijidanganya kuwa tunjua sana soka.Tuamketuwe na timu za vijana tuwe na mipango kwa ajili ya maendeleo ya taifa letu katika nyanja hii muhimu kabisa ya soka.Soka ni kazi kama kazi nyingine na si mahalapawatu waliokosa kazi kuwa sehemu ya kupakimbilia jamani.Soka ni ajira kama zilivyo ajira zingine soka ni kazi soka ni vita sokani mipango ya kweli na uhakika na si kuwa na mipango ya kikomedi. Soka Watanzania wenzangu ni kujitoa kwa halina mali.Hatujachelewa na tuanzse sasa.Asanteni.

Thursday, November 29, 2007

WATANZANIA KUNDI LETU NDILO GUMU WALA SI RAHISI!

Kuna baadhi ya watu wameanza kuwadanganya watanzania nasi watanzania ni wepesi wa kuamini mambo ambayo kwa hakika huwa si ya kweli kabisa!Kumbuka jinsi watu walivyokuwa na matumaini ya kwenda Ghana kila mmoja alijua kuwa mwakani sote macho yetu kideoni tukiwashangilia Stars na Stars nao masikini wakaanza kuvimba vichwa wakati hata safari bado ilikuwa mbichi kabisa!Kumbuka jinsi walivyokuwa na nyodo wakati wanakwenda kucheza na Zambia kule mji unaotamani angalau kuwa na bahari japo kwa siku moja,Morogoro,washabiki waluguru wale wamefika Msamvu kuwalaki wachezaji wao lakini Stars wakawafungia vioo maana tayari wao wameishakuwa wafalme!
Ninachotaka kusema siyo kukatisha tamaa la hasha bali kuwaasa watanzania wenzangu kuwa kundi letu si rahi ni gumu sana na pengine ndilo kundi gumu kuliko makundi yote katika safari hii ya kuwania tiketi ya kucheza kombe la dunia.
Tukumbuke kuwa kwa soka la kisasa hakuna kitu kinachoitwa timu rahisi au kundi rahisi kama nilivyosema jana kuwa mpira ni mchezo wa maandalizi kama mitihani,mpira ni mchezo wa kujitoa,kujituma,kupambana na si kucheza soka ya midomoniambayo ndiyo tunayoiweza watanzania.Mpira ni burudani lakini kwa upande mwingine mpira ni vita tena ni vita kubwa sana sana.Sitaki kuongea mengi leo maana nitakuwa kama nimemeza kanda na maneno yanajirudia yaleyale.Kwa kifupi tuache maneno tuanze maandalizi sasa wakati ni huu na wala hatujachelewa.Asanteni sana na ni matumaini yangu kuwa sote kwa pamoja tutashikamana na kuanza maandalizi sasa.

Wednesday, November 28, 2007

CAMEROUN WANAFUNGIKA IWAPO TU...............

Wasomaji wangu wapendwa kwanza naomba niwaombe radhi kwa kutokuwepo hewani kwa takribani mwezi hivi hii yote inatokana na kuzidiwa na majukumu.Naomba radhi sana kwa hilo.Najua dada Salome wa Mtibwa Sukari,Deogratius Zegge wa Serena pale Tengeru Arusha na Mwandishi wa siku nyingi wa "gazeti la Daily Vision" la Kantalamba Sekondari pale Sumbawanga 1991-1993 bwana Boaz A. Boaz mtakuwa menisamehe baada ya kuwa sijaonekena kwa muda mrefu kidogo.
Leo nataka nizungumze juu ya kupangwa kwa ratiba ya kombe la dunia Afrika Kusini 2010 kule Afrika ya Kusini.Tupo kundi la kwanza katika kanda hii ya Afrika pamoja na vinara Cameroun,Visiwa vya Cape Verde na Mauritius.Kimahesabu kundi letu ni kama rahisi sana lakini kimchezo ni kundi la kati au wastani au kundi la kama watu wengine waonavyo la hizi timu tatu kuwa wasindikizaji wanaomsindikiza mfalme Indomintable Lions.
Mpira ni mchezo wa maandalizi,juhudi,maarifa kujitoa,kujituma na pia mchezo wa makosa.Cameroun wanajielewa kuwa wao ni wababe lakini kamwe hawawezi kjidanganya kuona kuwa timu kwazo walizopangiwa nazo ni vibonde.Tukumbuke kuwa hawakuwepo Ujerumani na wanalitambua hilo na wanajua machungu ya kukosa kushiriki fainali hizo kwa wao kukosa penati nyumbani.Hawatakubali kufungika na wanaweza kuwa na hasira sana hasa ukizingatia kuwa hwakuwepo katika fainali zilizopita kama kawaida yao.Hawawezi kukubali wazikose fainali hizi tena zinazochezwa katika bara hili la hapa nyumbani.Kwa kifupi Wana Wa Cameroun wanatambua kuwa kundi walilopangwa nalo kwa soka la siku hizi si timu vibonde hivyowako tayari kupigania nafasi yao kuliko vile watu wengine wafikiriavyo kuwa wamepangiwa timu vibonde!Wana EWa Cameroun wataingia kupigana na wanajua kuwa nguvu ya adui zao ni kubwa kutokana na soka la siku hizi kuwa limekuwa sana.Halikadharika hizi timu zingine pia zinajua kuwa yupo mfalme wa kundi nasi pia tujitahidi tuzifunge timu zingine!Kifupi kundi letu kila timu inapiga hesabu za kivyakevyake ili waweze kufanikiwa.
Ninachotaka kusema ni kuwa Cameroun wanafungika lakini wanafungika tu iwapo tutaanza maandalizi mapema tutaanza maandalizi sasa hivi tutaanzana maandalizi leo na wala siyo kesho!Cameroun atafungika tu iwapo tutaacha malumbano ya kuwa wachezaji gani ni bora na wachezaji gani siyo bora!Cameroun atafungika tu iwapo tutashikamana wote na pia tutampa mwalimu sapoti kubwa sisi sote kama watanzania na tunoitakia mema timu yetu.Maandalizi yaanze sasa kupata mafunzo nje ya nchi,kupata mechi za majaribio kutokukata tamaa sote lazima tushikamane kwa umoja wetu tutaiweza safari ya Afrika Kusini na Angola 2010 na hakika tunaweza kuishangaza dunia.Watanzania hakuna lisilowezekana katika sayari hii ni mipango madhubuti na mikakati ya maana tu ndiyo itakayoweza kutukomboa kutoka katika utumwa wa kuwa wasindikizaji."TUJIKWAMUE SISI WENYEWE KUTOKA KATIKA MAWAZO YA KUWA WASINDIKIZAJI HAKUNA ATAKAYETUFANYA KUWA HURU ILA NI SISI WENYEWE!"
Boaz,Salome na Deo nisaidieni kuwaeleza watanzania kuwa haya mambo yanawezekana iwapo tutakuwa na maandalizi ya maan akutoka sasa.Naomba mnisaidie kuwaeleza watanzania wote!Nisaidieni kwa njia mbalimbali kwa kupiga kelele kwa vipeperushi,kwa kuwajulisha watu mbalimbali na kwa kutumia njia zozote zile kwazo zinafaa kufikisha ujumbe kwa jamii ya watanzania.Kombe la dunia inawezekana!TWENDE TUJIANDIKISHE SASA WAKATI NI HUU!
Mwaka 2010:
Nchi:Afrika Kusini
Mji:J'burg
Uwanja:FNB Stadium
Kundi A:Mabingwa Italy,Spain,Japan,Tanzania
Mechi ya ufunguzi:Mabingwa Italy vs Tanzania
Matokeo ya mechi:Tanzania 1-Italy 1.
Tanzania leo imetoka sare na mabingwa wa dunia Italia kwa kufungana bao 1-1 katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa First National Bank mjini J'burg katika mechi ya kwanza ya ufunguzi wa kombe la dunia hapa katika bara la Afrika.Ikumbukwe kuwa nchi hii ya Tanzania ndiyo mara yake ya kwanza kushiriki fainali hizi za kombe la dunia na pia ndiyo mabingwa wa kombe la Afrika kwa mwaka huu walilolitwaa mapema mwaka huu katika fainali za mataifa huru ya Afrika huko Angola baada ya kuwafunga mabingwa watetezi Misri huko mjini Luanda Angola.Mechi zijazo za Tanzania ni dhidi ya Japan na halafu itamalizia mechi zake kwa kupambana na Spain.
Hya mambo jamani yanawezekana ni suala la maandalizi tu na mipango madhubuti.Hakika inawezekana kama tumedhamiria na kama kweli tunataka kuwa washindani wa kweli.Asanteni sana na shime tuanze maandalizi sasa wakati ni huu bado hatujachelewa.